Crispin Materu ndio anajitengenezea utajiri wake mdogo mdogo kwa kuuza maua

Hakuna mtu asiyependa maua, maua hutumika kama kivutio kikubwa cha maeneo mbalimbali, kila nyumba utakayo itembelea utakuta maua ndani ya nyumba au nje ya nyumba, kila sherehe au kumbi za mikutano utakuta maua hii ni ishara tosha kuwa maua ni muhimu na yanahitajika.

Image result for miche ya maua biashara

Vijana wengi Tanzania wamejiajiri katika biashara hii ambayo imekua mkombozi wa maisha yao ambapo kwa mtaji mdogo wa mche mmoja wa Sh 500 ukazalisha miche 1,000 unapata faida ya Sh 500,000.

Kama kijana Crispini Materu anayefanya biashara hiyo maeneo ya Vatican Sinza, ambaye anadai kuwa hawezi kuacha biashara hiyo kwani ndio inayomweka mjini.

Alianza na mtaji mdogo alionunulia mbegu za maua na kuotesha na sasa anafanya biashara hiyo kwa miaka kadhaa na kujipatia maslahi ya kuendesha maisha yake mjini na kusaidia faamilia yake.

Anasema kuwa alijifunza kazi hiyo kwa baba yake mdogo aliekuwa akiishi Olasiti, Arusha aliekuwa akifanya biashara hiyo na kuuza maua yake katika sehemu mbalimbali pamoja na nje ya nchi.

Image result for maua biashara

Anasema kuwa zipo mbegu za maua ambazo hupatikana kwa urahisi kazi yako inakuwa kupandikiza au kuotesha .

Akielezea faida ya uuzaji maua anasema zipo faida mbali mbali unazoweza kunufaika nazo kwa biashara hiyo.

Mfano unaweza kuzarisha miche elfu moja na kila mche unaweza kuuza kwa bei tofauti kulingana na hadhi ya ua lenyewe.

Image result for miche ya maua biashara

“Jaribu uchukulie bei ya sh,500 kwa mche na uzalishe miche 1000 utapata kiasi cha sh,500,000 kumbuka hiyo ni bei ya makadirio ya chini waza kwa yale maua yanayouzwa mche 1500 na kuendelea”.

Pamoja na faida zake zipo changamoto mbalimbali kama ukosefu wa maji ya kutosha na uhaba wa wateja kwa wakati pale maua hayo yanapofikia hatua ya kuyauza na nyingine ni uharibifu wa maua hayo.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com