Umetumia sukari leo? Basi huwezi kuzuia mwili wako kufanya hivi.

Voice: Abdulkidee

Imagine umetafuta nafasi ya kazi muda halafu siku ya interview unachelewa kuamka unachelewa interview halafu unashindwa kupata dili. Ungejisikiaje? Imagine kama safari zako zote za majaribio ya mahaba zinagekua zinaishia Foreplay. Pale ambapo umejiandaa sana kula nyama na kisu unacho lakini ni butu mbaya…Crazy huh!.

Pamoja na sukari kufanya chakula kiwe kitamu, Inasaidia chakula kisiharibike mfano cake, inasaidia kuhifadhi maji kwenye tunda, inabalance acid kwenye tomato source na pia inasaidia kuongeza kuweka texture na ladha kwenye misosi mingine kibao.

Yako mengi maovu yanatokea mwilini kama wewe ukizidisha kiwango cha sukari, lakini kwa haraka ni kwamba heart attack (Presha), diabetes (Kisukari) , unene kupitiliza (Obesity) , ni baadhi tu ya vitu sukari inasababisha. Kubwa zaidi ni sukari inazuia utendaji kazi wa kinga ya mwili. Inazuia uzalishaji wa antibiotic, inazuia usafirishaji wa vitamin c, na kuendelea.

Lakini; Hata kama ukijua madhara yote haya, Je utaacha kukata kiu yako ya chocolate, au soda baridi? Je cake? Ni ngumu sana kuacha kitu pekee kitamu zaidi katika maisha ya binadamu.

So kama utaendelea kutafuna endelea; Ila shirika la afya duniani Mwaka 2015 lilipitisha Kiwango ambacho mtu anapaswa kutumia sukari kisizidi 12 teaspoon.

Na nchini Marekani pia shirika la AHA lilipitisha kiwango cha vijiko vya chai 9 kwa mwanaume na vijiko 6 kwa mwanamke. Hii inaweza kukusaidia katika kuimiliki afya yako izuri. Sukari ikizidi mwilini haya ndio mambo yanayoharibika.

You may also like...

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com