Listen Live!

Jifunze kuuza product yako Exclusively. Use Nipsey Hustle trick. – Audioblog

Audio: Abdulkidee

Kwenye uwanja wa biashara ya Hip Hop na rap Top 5 ya wenye pesa nyingi zaidi mpaka mwaka 2018 imeongozwa na Jay z, Didy, Dr Dre, Eminem, na Drake. Sijui imekuaje kwa 50 cent. Hawa ndio jamaa walioko meza kuu ya mapato ya kimuziki.

Jay z, ndio tajiri zaidi kwenye muziki wowote hivi sasa, lakini kuna maingizo mapya ambayo ndio yanachanua. Chance the rapper na Currency hawatakosekana kwenye list.

Marehemu Nipsey Husttle yeye ni wa aina yake na katika hizi list mbili ya wale wa juu zaidi na hawa wapya yeye atafaa kukaa katikati hapo.

Sio kwamba jamaa alikua tajiri kupindukia lakini kwa vile Nipsey alikua na akili ya kipekee katika utafutaji na alifanikiwa kufanya moves ngumu kwa kuuza muziki na kufanikiwa kipekee.

Kwanza Nipseey amekua kwenye game tyangu mwaka 2005 alipotoa Mixtape yake ya Nipsey Hustle. Akachapa colabos kwa miaka hiyo Snoop Dog, Drake na wengine kibao. Lakini alitisha zaidi baada ya kuondoka kwenye dili yake na Epic Records ana akaanzisha Record Lebel yake All Money IN.

Aliachia Mixtape ya kwanza akisimamia mwenyewe, ikafanya vizuri sana. Siri kubwa ya kumtofautisha Nipsey ana watu wengine ni mbinu zake za tofauti za ku-market bidhaa zake kwa ubunifu na mafanikio.

Alipoona watu hawanunui tena records na yeyey anataka kuuza, akaamua kuuza copy 1000 tu Exclusive, kwa $100. Mchezo huu ulimsisimua Jay Z mpaka akaamua kumuunga jamaa mkono kwa kuspend Ksh 1,000,000 (Tsh 22 milion) kununua copy 100 mwenyewe.

Nipsey alitengeneza $100 X 1000 kumbe mwana alitengeneza 100000 ndani ya siku moja. Mpango wake huu aliuita Proud 2 Pay.

Baada ya mafanikio ya mkakakti huu kwenye mauzo ya kazi zake, Nipsey aliendelea kutumia ujanja huo na kuuza album na mixgape kadhaa baadae.

Nipsey alilijulia soko lake vizuri, na hii ndio inamfanya awe tofauti sana na wasanii wengi. Alipotengeneza Copy 1000 na kuziweka sokoni kama Limited edition. Alifanya promo kali ambalo liliwafanya watu watamani kuwa na copy hizo Limited ambazo hazitapatikana sehemu nyingine yoyote kwa watakaokosa.

Idea hii amewahi kusema kwamba aliipata kutoka kwa mwandishi Jonah Burger ambaye alisema kuhusu mgahawa unaocharge raia $100.  Jamaa ameitest idea ambayo iko kwenye kitabu na ikafanya kazi kwake.

Baada ya hapo Nipsey akaendelea kuafnya vizuri hata kwenye mishe mishe zake nyingine. Mfano alipomiliki aina yake ya weed.

Ni msanii ambaye ametoa inspiration kubwa sana kitaani.

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com