Sasa hutahitaji tena koti msimu wa baridi, unahitaji aina mpya ya kitambaa inayotengeneza joto.

Voiced by @Abdulkidee

Habari nzuri kwa akina dada ni kwamba, sasa unaweza kuvalia nguo tight hata kama kuna baridi kali sana. Si mnapenda kubana mwili kidogo?

Kampuni ya Mitsubishi chemical corp, ya Japan imeunda aina mpya ya kitambaa laini sana ambacho nguo zake zitafaa ku-replace uvaaji wa masweta na makoti msimu wa baridi kali, kwa kuwa kinatengeneza joto na kukufanya usihitaji sweta. Kitambaa hicho ambacho kimepewa jina la “Celwarm” ni laini na kinaondoa kabisa sababu ya mtu kuvaa manguo mengi ili kujikinga na baridi.

Nguo zilizotengenezwa na kitambaa hiki kwa mara ya kwanza zimeanza kuuzwa mwezi August 2019, na zinatarajiwa kuuzwa zaidi katika msimu wa Global Shopping Festival inayofanyika November 11 2019.

Kitambaa hiki cha ”Celwarm” kinaweza kutengeneza joto kwa kutumia chembe maalum zinazodaka miale kutoka kwenye jua na kuihifadhi, pamoja na miale maalum inayotolewa na Incandescent bulb, “zile bulb za kawaida kabisa” hivyo kukufanya kuwa na uhakika kwamba hata kama ukilikosa jua joto liko palepale kwa sababu utatumia bulb. Kitambaa hiki ni laini, confortable na sio rahisi kuamini ndio koti lenyewe hilo.

Kampuni za China, Japan ana nchi zingine zenye uzalishaji mkubwa wa bidhaa za mavazi na fashion zimekua zikitumia kiasi kikubwa cha pesa kufanya tafiti ili kujua wateja wanataka vitambaa vya aina gani nan a wao hutengeneza. Kampunui kama Tmall zinatumia Trend forecasting centre kukamua insights kutoka kwenye data kubwa, jambo linalowapa nguvu ya kubaki vinara wa soko la nguo na fashion China na duniani. Hatua hii ni muhimu sana kwenye mafanikio ya kampuni za sasa, kutokana na kuwepo kwa wingi wa bidhaa ambazo mteja anaweza kuchagua.

Pamoja na kwamba soko la nguo nchini China ni kubwa pengine kuliko sehemu nyingine duniani, idadi ya viwanda na wazalishaji ni wengi sana pia. Brand na kampuni kubwa zinahitaji kutumia effort kuweza kupata sales nzuri. Zipo kampuni kutoka Japan, Korea mpaka Ulaya na Marekani ambazo zinapambania soko la China, hivyo Yule anayelegea kidogo basi watu wanakula.

Endelea kufuatilia watupipo kwa information zaidi kuhusu biashara na maisha na mishe mishe za watupipo

Watupipo

I am the moderator.

You may also like...

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com