Listen Live!

Ikiwa unahitaji perfomane, basi tafuta hizi mbegu Kariakoo.

Hizi mbegu hapa zinajulikana kwa jina la Nutmeg (bado sijajua jina la kiswahili) hutumika kama viungo na kuongeza ladha katika chakula lakini pia ni moja kati ya dawa poa sana ya asili. Zina uwezo wa kuondoa gesi tumboni, kuzuia kuharisha, kuponya au kupunguza maumivu ya viungo, kumaliza maumivu ya tumbo, kumaliza kichefu chefu (nausea) na hata hutumika katika kutibu kansa.

Lakini kama husumbuliwi na hayo hapo juu, utahitaji kujua kwamba mbegu hizi zinaweza kukuongezea libido na perfomance kwenye shughuli za kindoa. Utafiti umethibitisha hili.

(Hizi hapa Nutmeg, zina ganda flani gumu sana)

Mbegu hizi pia zinaweza kusaidia kuweka sawa mfumo wa hedhi (menstruation) kwa wanawake.

Nutmeg pamoja na udogo wake imejaa kiasi kikubwa cha antioxidants kama vile plant pigments, pamoja na aina muhimu ya mafuta.

Antioxidants ndani ya mbegu hizi zinasaidia mwili kudili na free radicals, ambayo ni hali inayohusishwa na usababishaji wa magonjwa kama cancer Alzheimer’s, kuzeeka na ishu nyingine kibao.

( Uzee hapa umetajwa kuchangiwa kwa kiasi fulani na mkusanyiko wa free radicals kwa kipindi kirefu)

Antioxidants kwenye mwili husaidia free radicals ku-stabilize (kukaa vizuri)

Kila mtu anazalisha free radicals nan i kitu ambacho huwezi kukikwepa. Lakini njia moja wapo ya kuzifanya zisiwe na madhara ni kuongeza kiwango cha antioxidants mwilini. Hapo ndio tunarudi pale kwenye mbegu yetu ya Nutmeg.

“Blah blah kuhusu mambo yanayoongeza kiwango cha free radicals ni yale yale maarufu na mengine hayakwepeki”

Uvutaji sigara

Unywaji wa Pombe

Misosi yenye sukari nyingi.

Hewa chafu

Baadhi ya dawa za wadudu kwenye mimea.

Mionzi na mengine mengi.

Sio kwamba unaambiwa uachane na matumizi ya vitu hivi, ila ukishajua unaweza kuongeza ulaji wa Nutmeg na vyakula vingine ambavyo vitasaidia kusawazisha damage zinazoletwa na mazaga hayo unayotumia. Mwisho wa siku ni chaguo lako tu.

Endelea kufuatilia watupipo na upite kwenye mitandao yetu ya kijamii Facebook, na Instagram. #Unleashyourbestself

You may also like...

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com