Listen Live!

Kiasi hiki cha pesa kinatosha kununua fadhila za mzazi wako?

Xi Lin (sio jina halisi) raia wa China ameamua kuuza kila kitu anachomiliki ili amrudishie mama yake pesa zake zote alizotumia kumlea hadi kufikia miaka 32.

Lin ambaye ni engineer alikua akiishi na mama yake ambaye alikua mkali sana. Katika siku zake zote za maisha mama yake alikua aki control karibu kila kitu anachofanya jamaa. Alimchagulia kozi ya kusoma, kazi ya kufanya kiasi kwamba jamaa hakuwa huru kabisa.

Ilifika wakati wa kujihusisha na mapenzi mama aka sugest mtu ambaye aliona anafaa kwa mwanae., wakaishi katika mahusiano kwa miaka kadhaa mpaka alipofika miaka 32 mahusiano yao yakavunjika. Siku moja akiwa katika mkutano kazini wakiwa katika mkutano, aliamua kuacha kazi hiyo hapohapo kwenye mkutano, akasimama na kuondoka bila hata kuaga.

Akaenda nyumbani kwake na kuuza kila kitu alichokua anamiliki na akaenda kumpatia mama yake kiasi cha dola 90 elfu ili tu amuachie uhuru wake, na jamaa akatoweka na hakuonekana kwa miaka kadhaa. Baada ya muda kupita huku baadhi ya jamaa wakiamini kwamba huenda jamaa aliuawa au kujiua, au pengine alitekwa, huku mama yake akisisitiza kwamba huenda ameingia kwenye madawa ya kulevya kupindukia

Siku moja jamaa aliamua ku-update status yake ya Facebook akaonesha kua yuko Seatle Marekani na anafanya biashara katika gari la kuuza chakula.

Unaonaje ishu ya mzazi kukufanyia kama alivyofanyiwa Lin? #Thinkaboutit

You may also like...

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com